DAWA ZA KUSISIMUA MISURI ZA PONZA WATU 90

 
Dawa za kusisimua misuli zimepigwa marufuku duniani hasa michezoni
Maafisa wa kupambana na dawa za kulevya nchini Marekani wamewatia mbaroni zaidi ya Watu tisini wakati wa msako wa maabara zinazojihusisha na dawa za kusisimua misuli.

Zoezi hilo lililofanyika katika majimbo ishirini lililenga dawa za kusisimua misuli ambazo zinatengenezwa na kusafirishwa kutoka China.
Mamlaka inayodhibiti matumizi ya madawa nchini Marekani,imesema Operesheni hiyo inayoitwa Cyber Juice imeanza mwezi Aprili na kulenga maabara zinazofanya kazi kwa siri zinazojishughulisha na dawa zinazopatikana kwa njia ya mtandao kutoka nchini China.
Zaidi ya uchuguzi kwa kesi 30 umesababisha kusitishwa kwa maabara kumi na sita ambazo zinajihusisha na dawa za kusisimua misuli.
Mawakala hao pia wamekamata poda inayotumiwa kutengeneza dawa hizo na fedha taslimu dola milioni mbili na rasilimali nyingine.
Msemaji wa mamlaka hiyo amesema kampeni hiyo ina lengo la kusitisha soko la chini kwa chini la dawa zilizopigwa marufuku, na kuweka bayana athari zake

Comments