DIAMOND ATANGAZWA KUWANIA TUZO ZA MTV EUROPE 2015

Msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ametangazwa kuwania Tuzo za MTV Europe “MTV EMA” kwa mara ya pili, Mwaka jana alitangazwa kuwania Tuzo hizi pia japo hakufanikiwa kushinda.

Diamond Platnumz ametangazwa kwenye kipengele cha ‘African Act’ ambapo anachuana na Davido, Yemi Alade, AKA na msanii mmoja ambaye atapendekezwa na mashabiki lakini ni kati ya Wizkid, K.O, Stonenwoy, Cassper Nyovest na Dj Arafat.
Tuzo hizo zitatolewa tarehe 25 mwezi October huko Millan nchini Italy

Comments