DOVUTWA AWATAMBIA LOWASSA NA MAGUFULI KWENYE MBIO WA KUWANIA URAIS

 

MGOMBEA urais kupitia chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, amesema atahakikisha anawapinga kwa hoja wagombea wenzake wa nafasi hiyo ili awapelekee ufunguo wa Ikulu waliomtuma.

Akizungumzia mikakati ya chama hicho, Dovutwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho alisema atahakikisha anapambana na mgombea wa CCM, Dk John Magufuli na Mgombea wa Chadema, Edward Lowassa .
“Nimewachagua wagombea hawa si kwa kuwa hakuna wagombea wengine bali viongozi wao wamekuwa wakisema eti ni wagombea mahiri, mimi nawaambia watakapobandua mimi nabandika, wakishuka mimi napanda,” alijigamba.
Alisema Lowassa ni kati ya viongozi walioweka mazingira magumu kwa vyama vya upinzani nchini, kwa kuvibana na kuvifanya vikose pumzi. “Magufuli tunafahamiana na Lowassa pia tunafahamiana lakini chama ninachokitetea hakitambui mahusiano yetu kwa hiyo nimetumwa niwapinge ili nipeleke ufunguo wa Ikulu uende UPDP,” alisema

Comments