KUBENEA KUMVAA DR.SLAA ASEMA ATAWEKA MAOVU YAKE WAZI WATANZANIA WAYAJUE
Katika taarifa yake kwa Mwanahalisi Online, Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL) wachapishaji gazeti la MwanaHALISI, (ambaye amechimba kwa undani sakata la Richmond lililotokea mwaka 2007) amesema:
NIMEMSIKILIZA
kwa makini, Dk. Willibrod Slaa, aliyeacha Ukatibu mkuu wa Chadema na
katibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) akizungumza katika
mahojiano na kituo cha telebisheni cha Star TV.
Dk.
Slaa ambaye ni msomi wa thiolojia, amemtuhumu Mgombea Urais
anayewakilisha UKAWA, Edward Lowassa kwamba ni fisadi na hafai
kuchaguliwa na wananchi.
Ikiwa
ni mara yake ya pili kutokeza hadharani tangu aliposusa kufanya kazi za
katibu mkuu katikati ya mwezi Julai mwaka huu, ameeleza kwanza
Watanzania wamchague “Mgombea mwenye nafuu ya ufisadi...” akamtaja John Pombe Magufuli.
Kwa
taarifa mpya aliyonayo na ambayo aliitumia katika mkutano wake na
waandishi wa habari Jumanne iliyopita, kuhusu sakata la Richmond,
aliipata kutoka kwa Dk. Harrison Mwakyembe, aliyekuwa mwenyekiti wa
kamati Teule ya Bunge, juu ya Richmond.
Kubenea
amesema ameshindwa kuvumilia taarifa anazozitoa Dk. Slaa kuhusu sakata
hilo na sasa ataeleza anachokijua kuhusu sakata la Richmond na msukumo
uliopo hata Dk. Slaa kujitokeza wakati huu wa kampeni za uchaguzi katika
mlengo wa kumshambulia na kumchafua Lowassa.
“Niliamua
kutojibizana na Dk. Slaa – rafiki yangu wa miaka mingi – katika mradi
wake huu. Lakini kwa hapa alipofika, uvumivu umenishinda. Sitaruhusu mtu
mzima, anayejiita padri na ambaye alitaka kuwa rais wetu, kuendelea
kulindanganya taifa na kuwapotosha wananchi.
“Hivyo
basi, nimeamua kuanzia leo hii, kukabiliana na Dk. Slaa kwa kila kona
ili ukweli ufahamike. Kwa kuanzia, leo hii – Jumamosi, naelekea mkoani
Mbeya ambako nitahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika jimbo
la Kyera, linaloshikiliwa na Mwakyembe, swahiba mpya wa Dk. Slaa.
“Nikiwa Mbeya nitaeleza ukweli wa kilichotokea na kile ambacho Dk. Slaa anakificha.
“Aidha,
nikirejea Dar es Salaam, nimepanga kuitisha mkutano na waandishi wa
habari, kueleza ukweli uliokamilika kuhusu Dk. Slaa na mkewe Josephine
Mushumbuzi na sababu ya yeye kususia chama.”
Comments
Post a Comment