MEMBE AWAONYA WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTO TOA MATAMKO KABLA YA NEC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema waangalizi wa uchaguzi hawatakiwi kutoa tamko lolote linalohusu uchaguzi au kampeni kabla Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) haijatangaza matokeo.
Akizungumza
jana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania, Membe alisema
waangalizi hao wanaweza kutoa ripoti zao baada ya kuthibitishwa na
wizara ya mambo ya nje, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) na Nec.
Membe
alisema waangalizi wote watakuwa huru kufanya kazi zao na serikali
itahakikisha kuwa wanakuwa salama muda wote watakapokuwa nchini. Amesema
waangalizi wa uchaguzi hawataruhusiwa kufika baadhi ya maeneo ambayo
yatabainishwa na Nec.
“Waangalizi
watapewa fomu na Tume za uchaguzi ili kuwatambua kama waangalizi wa
uchaguzi. Hawataruhusiwa kufanya kazi zao kwenye baadhi ya maeneo, kwa
mfano maeneo ya kijeshi na mengine,” alisema waziri huyo
Amewataka
waangalizi kutofungamana na upande wowote, badala yake wafanye kazi yao
bila kuingilia mchakato wa uchaguzi wa Oktoba, 25. Amesisitiza umuhimu
wa amani wakati wa uchaguzi na kuwataka waangalizi hao kutokuwa chanzo
cha vurugu.
Comments
Post a Comment