TANZANIA KUKAA GIZA KWA WIKI NZIMA
BAADA ya kufika kwa gesi asilia jijini Dar es Salaam ikitokea Mtwara, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), itaingiza gesi hiyo katika mitambo yote ya umeme nchini, hivyo kuanzia leo kutakuwa na ukosefu wa umeme katika mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa.
Hatua
hiyo inatokana na kuzimwa mitambo yote ya umeme katika kituo kikubwa
cha kuzalisha umeme cha Ubungo, Dar es Salaam kwa nia ya kuingiza gesi
asilia katika mitambo huo.
Imeelezwa kuwa tatizo hilo la umeme, litadumu kwa wiki nzima ambao umeme utakatika kwa saa kadhaa usiku na mchana, lakini hali itakuwa mbaya zaidi kwa siku ya leo.
Imeelezwa kuwa tatizo hilo la umeme, litadumu kwa wiki nzima ambao umeme utakatika kwa saa kadhaa usiku na mchana, lakini hali itakuwa mbaya zaidi kwa siku ya leo.
Akizungumza
katika kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi One jana, Mkurugenzi
Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema mitambo yote ya umeme
itazimwa ili kuingiza gesi asilia kuanza kuzalisha umeme katika kituo
hicho kikubwa.
“Wiki
hii umeme utakatika sana kutokana na kuunganishwa gesi kutoka Mtwara
kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa kuanzia kesho mitambo yote itazimwa,” alisema Mramba.
Alisema kwa saa za mchana na usiku ndani ya wiki hii itakuwa mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa itakosa umeme.
Alisema kwa saa za mchana na usiku ndani ya wiki hii itakuwa mikoa yote inayotumia Gridi ya Taifa itakosa umeme.
Alisema
baada ya majaribio ya kupitisha gesi asilia kukamilika sasa wanaingiza
kwenye mitambo hiyo ili kuanza kuzalisha megawati 150 za umeme huku
mitambo ya megawati 200 iliyokuwa haifanyi kazi kutokana na gesi
kutotosha nayo itaanza kufanya kazi.
Alisema
baada ya kuunganisha bomba hilo na umeme kuanza kuzalishwa mwishoni mwa
wiki Watanzania watakuwa na uhakika wa umeme pamoja na bei ya umeme ya
uhakika kwa muda mrefu.
“Kutokana
na kuwa na gesi ya uhakika naamini mdhibiti ataangalia na bei inaweza
kupungua ingawa siyo kesho au mapema,” alisema bosi huyo wa Tanesco.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk James Mataragio alisema kwa sasa mitambo ya
Kinyerezi imejaa gesi na wameishaingiza gesi yenye mgandamizo wa tatu
na inatakiwa kufika mgandamizo 50 hadi 51 ili kuzalisha umeme.
Alisema
kwa muda wa wiki watakuwa wamefikisha mgandamizo huo kwa kuingiza
polepole baada ya kufanya majaribio na kuona kuna uwezo wa kuingiza
mgandamizo 90.
“Kuanzia
kesho (leo) mpaka baada ya wiki mbili tutakuwa na uwezo wa kuzalisha
umeme kwa gesi kwa kufikia mgandamizo huo wa 50,” alisisitiza na
kuongeza kuwa uzalishaji huo, Serikali itaokoa dola bilioni moja
zilizokuwa zikitumika kwa uzalishaji umeme wa mafuta.
Mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam ulikamilika Julai mwaka huu.
Comments
Post a Comment