WAANDAMANAJI WAFANYAVURUGU UTURUKI
Maelfu ya waandamanaji waliokuwa wakipepea bendera za Uturuki wamevamia makao makuu ya chama kikuu cha Kikurdi cha HDP.
Jengo hilo lililoko katika mji mkuu wa Ankara baada ya kuvamiwa lilichomwa moto.
Chama
hicho baadaye kilitoa maelezo kwamba majengo yake mengine yaliyoko
kwenye miji mingine yalilengwa pia,mjini Kabul ambamo ziko ofisi za
gazeti moja la Hurriyet zilishambuliwa kwa mara ya pili katika kipindi
cha wiki mbili .
Naye waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu
amelaani vikali mashambulizi na uvamizi huo katika ofisi za kisiasa na
hata kwa nyumba za habari na ametoa wito wa kusitisha ghasia.
Mpaka
sasa askari jeshi kumi na wanne wa Uturuji wanaarifiwa kupoteza maisha
mapema wiki hii katika shambulio la bomu upande wa mashariki mwa nchi
hiyo.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema majeshi yake yatapambana na magaidi wa nchi hiyo.
"Hatujaacha
matarajio ya watu wetu na hatutaacha kwa magaidi, kwa makundi ya
wanaotaka kuipindua nchi na washirika wao. Uturuki ambaye
imewezakushinda mambo mengi hapo nyumba hadi sasa, itashughulikia suala
la magaidi. Nchi yetu na wanajeshi wake, polisi na maafisa ujasusi
wanajitahidi kupambana na makundi ya kigaidi nayogawa nchi pamoja silaha
zao. Hadi sasa uharibufu mkubwa umefanywa na makundi hayo, kutoka ndani
na nje ya mipaka yetu. matukio ya hivi sasa ni ya ziada, na
kuchanganyikiwa kwa makundi hayo ni jambo tulilolizoea." amesema
Erdogan
Comments
Post a Comment