WELBECK KUWA NJE YA UWANJA MPAKA DISEMBA
Mshambuliaji wa
klabu ya Arsenal Danny Welbeck atakuwa nje ya Uwanja mpaka mwezi Disemba
baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye Goti .
Arsenal imeeleza kuwa matibabu kwenye Goti hilo hayakwenda vizuri na Wiki iliyopita ikaamuliwa afanyiwe operesheni.
Welbeck, aliumia Goti lake mwezi Aprili huku akiwa kaifungi timu yake ya Arsenal mabao 8 katika Mechi zake 34 tangu ahamie hapo kutoka Man United.
Hili ni pigo kubwa kwa Arsenal ambayo haikusajili mshambuliaji . Dirisha la usajili la kiangazi lilifungwa jumanne iliyopita.
Mfaransa Oliver Giroud anabaki kuwa mshambuliaji pekee wa kutumainiwa katika kikosi hicho.
Comments
Post a Comment