ASKARI ALIYE KUWA AKIONGOZA MSAFALA WA MAGUFULI AFARIKI DUNIA


Askari wa usalama barabarani aliyekuwa akiongoza msafara wa mgombea urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli amefariki dunia baada ya kugongana na dereva bodaboda katika eneo la Ubungo jijini Dar es salaam.

Mkuu wa polisi kitengo cha usalama barabarani DCP Mohamed Mpinga amesema askari huyo alikuwa kwenye pikipiki maalum iliyokuwa ikiongoza msafara wa Dkt Magufuli, ambaye alikuwa akitokea katika hospitali ya Lugalo kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe.

Kwa mujibu wa Kamanda Mpinga, tukio hilo limetokea majira ya saa 6 mchana ambapo msafara huo ulikuwa ukielekea maeneo ya Uwanja wa Ndege, na kwamba dereva bodaboda aliyegongana naye amenusurika kifo.

Comments