CCM WALALAMIKIA KITENDO CHA MAALIM SEIF HAMAD KUJITANGAZA MSHINDI ......WADAI WALIKAMATA KURA FEKI ZA CUF
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema, Maalim Seif amevunja katiba na sheria kwa kujitangaza mshindi kabla ya matokeo halali ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec).
Akizungumza
na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho Kisiwandui,
mkoa wa Mjini Magharibi Unguja jana, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho
Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya
mwaka 1984 na sheria namba 11 ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, hakuna
chombo chochote chenye mamlaka ya kutangaza matokeo zaidi ya Zec.
Alisema
bila ya hekima na busara za wananchi, kitendo hicho kingeweza
kusababisha uvunjifu mkubwa wa amani na kuitaka Zec kuchukua hatua za
kisheria dhidi ya mgombea huyo wa urais wa Cuf.
“Tumesikitishwa
sana na Zec kushindwa kuchukua hatua ikiwamo kukemea kitendo cha
mgombea mmoja kujitangaza mshindi kati ya wagombea 14 wanaowania nafasi
hiyo. Tunaomba Tume ya Uchaguzi ifanyekazi kwa mujibu wa katiba na
sheria bila ya kumuogopa mtu yoyote,” alisema.
Katika
mkutano huo, Vuai aliambatana na Spika wa Baraza la Wawakilishi
aliyemaliza muda wake. Pandu Ameir Kifichio, Waziri Kiongozi Mstaafu
Shamsi Vuai Nahodha,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Vikosi vya SMZ na wajumbe wa timu ya kampeni ya mgombea urais wa CCM
Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Aidha,
alisema CCM imesikitishwa na tukio la kukamatwa karatasi bandia za
kupigia kura katika Jimbo la Chonga, mkoa wa Kusini, Kisiwani Pemba.
Comments
Post a Comment