HUU HAPA UHAKIKA KUHUSU MH. JUMA MWAPACHU KUJIVUA UANACHAMA CCM
Kuna stori ambayo imesambaa tayari kwenye Mitandao ya Kijamii ikimhusisha mmoja ya Wanachama wa CCM, Balozi Juma Mwapachu kuhama CCM… Kuna ukweli wowote?
Taarifa iliyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi imethibitisha Balozi Juma Mwapachu kutangaza kujitoa CCM >>> “MWAPACHU
ATOKA CCM: Kada wa CCM Balozi Juma Mwapachu leo ametangaza kujivua
uanachama wa chama hicho, adai chama kimepoteza dira, hajaamua kujiunga
chama kingine“>>> Hiyo ni nukuu ya stori iliyoripotiwa na gazeti la Mwananchi.
Kwenye ukurasa wa Twitter wa Kituo cha Television cha ITV nako imeripotiwa taarifa hiyo >>> “#Habari Balozi Mwapachu ametangaza rasmi kuanzia kesho hatokuwa mwanachama wa CCM na atarejesha kadi ofisi ya CCM kata ya Mikocheni DSM” >>>@ITVTANZANIA
Hizi hapa ni post ambazo zimesambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii kuhusu stori hiyo.
Comments
Post a Comment