KADA WA CCM AMWAGIWA TINDIKALI


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana Chadema kata ya Sirari na kuhamia chama cha CCM, Weng’ari Mang’era (26) amemwagiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati wakimpokea mgombea ubunge wa Tarime Vijijini(CCM), Christopher Kangoye  katika uwanja wa Tarafa Sirari Wilayani Tarime.

Shuhuda mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe ameeleza” Mbunge Kangoye alikuwa anakwenda kwenye mkutano Uwanja wa Tarafa  wakati tuko barabarani  watu   wakafika na kumjeruhi kwa kumwagia tindikali,’amesema.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Lazaro Mambosasa amesema polisi wanafuatilia kujua  waliohusika na tukio hilo.

Wakati hilo likitokea, Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Athuman Akalama  alisimamisha kampeni kwa wagombea zilizokuwa zinaendelea Nyamongo baada ya kuibuka kwa vurugu kati ya CCM na Chadema.

Leo asubuhi mgombea Udiwani Kata ya Matongo-Nyamongo(CCM), Daud Itembe akiwa kwenye harakati zake za kuhitimisha kampeni zake   zilizokuwa zifanyike maeneo ya stendi Nyamongo ziliibuka vurugu kati ya wafuasi wa CCM na Chadema

Comments