KILIMANJARO YAVUNJA REKODI ..,,,.,.,.,.MAJIMBO 7 KATI YA 9 YACHUKULIWA NA UKAWA
Mkoa wa Kilimanjaro, umevunja rekodi ya uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 baada ya upinzani kunyakua majimbo saba kati ya majimbo tisa.
Mwaka
1995, upinzani ulinyakua majimbo sita ya Hai,Siha,Rombo, Moshi
Vijijini, Moshi mjini na Vunjo na kuiachia CCM majimbo ya Mwanga, Same
Mashariki na Magharibi.
Lakini
kati ya mwaka 2000 na 2010, CCM ikafanikiwa kukomboa majimbo ya Siha na
Moshi Vijijini lakini katika uchaguzi wa 2015, majimbo hayo yameangukia
tena mikononi mwa upinzani.
Mbali
na majimbo hayo, katika historia ya vyama vingi, safari hii upinzani
umejipenyeza katika jimbo la Same Mashariki ambalo lilikuwa ngome ya CCM
na kuwa miongoni mwa majimbo ya upinzani.
Majimbo
ambayo sasa yanashikiliwa na upinzani ni Hai,Siha,Moshi Vijijini,Moshi
Mjini, Vunjo, Rombo na Same Mashariki huku CCM ikibaki na majimbo mawili
ya Mwanga na Same Magharibi.
Katika
tukio lingine, aliyekuwa mgombea Ubunge Jimbo la Moshi mjini kwa tiketi
ya CCM, Davis Mosha, amempongeza mpinzani wake, Jaffar Michael wa
Chadema kwa kupata ushindi wa kishindo.
Michael
aliibuka na ushindi wa kura 51,646 dhidi ya kura 26,920 alizopata
Mosha, na hivyo kumfanya Michael ambaye ni Meya wa mji wa Moshi
aliyemaliza muda wake kutangazwa mshindi.
Juzi
saa 4:26 usiku, Mosha alimtumia Michael ujumbe mfupi wa maandishi
(SMS), akimpongeza kwa ushindi wa kishindo, kitendo ambacho hakijawahi
kutokea katika historia ya jimbo hilo.
“Mhe Japhary Michael nachukua nafasi hii kukupongeza kwa ushindi wa kishindo katika nafasi ya Ubunge Jimbo la Moshi,”alisema Mosha ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara matajiri nchini.
“Najua
kuna sehemu tulikwaruzana ama kuhitilafiana kwa maneno. Hiyo ilikuwa
siasa sio ugomvi binafsi nisamehe na Mungu akubariki. Kama utahitaji
msaada wowote tafadhali tuwasiliane,”alisema.
Comments
Post a Comment