LOWASSA TAYARI KASHAPIGA KURA LAKINI ATOA ANGALIZO KUHUSU MATOKEO


Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Edward Lowassa amepiga kura, Monduli 
Lowassa  alipata  nafasi  ya  kujibu  maswali  kadhaa  ya  waandishi  ambao  walitaka  kujua  kama  atakuwa  tayari  kutakubali  matokeo  iwapo  atashindwa.
 
Katika  majibu  yake, Lowassa  amesema  atakubali  matokeo  kama  hayatachakachuliwa, vinginevyo  hatakubali.
Waandishi  pia  walitaka  maoni  ya  Lowassa  kuhusu  hukumu  ya  mahakama  kukataza  watu  kukaa  mita 200  baada  ya  kupiga  kura.
Katika  majibu  yake, Lowassa  amesema  hali  aliyoiona  kituoni  ni  ya  amani  na  utulivu  hivyo  hana  maoni  ya  ziada  kuhusu  hukumu  ya  kukaa  mita  200

Comments