MAHUJAJI WA TANZANIA WALIOFARIKI WAFIKIA 22
Idadi ya raia wa
Tanzania waliofariki katika mkanyagano wakiwa katika ibada ya Hajj
nchini Saudi Arabia mwezi uliopita
imeongezeka na kufikia 22,kulingana
na waziri wa maswala ya kigeni.Mwandishi wa BBC Leonard Mubali anasema kuwa mahujaji wengine 38 kutoka Tanzania hawajulikani waliko.
Serikali ya Saudia imesema kuwa takriban watu 769 walifariki katika mkanyagano ,ijapokuwa maafisa kutoka mataifa wanayotoka mahujaji waliofariki wanasema kuwa idadi hiyo ni watu 1,480.
Comments
Post a Comment