MAJAJI 7 WASIMAMISHWA KAZI KWA UFISADI HUKO GHANA
Majaji saba wa mahakama ya juu nchi Ghana kati ya 12 wamesimamishwa kazi kwa mda kufuatia madai ya kuhusika katika ufisadi.
Mwezi uliopita majaji wengine 22 wa ngazi za chini walisimamishwa kazi baada ya filamu moja kuwaonyesha wakichukua hongo kutoka kwa wateja ili wapate kupendelewa katika kesi.
Filamu hiyo ilizua hisia kali wakati ilipoonyeshwa mara ya kwanza mjini Accra.
Majaji wengine kadha wamekataa madai hayo na kwenda mahakamani kupinga kusimamishwa kwao kazi.
Saba hao walikuwa na kesi ya utovu wa nidhamu kufuatia makala yaliyoandaliwa na mwandishi Anas Aremeyaw.
Mwandishi huyo anamiliki ukanda wa video wa takribam saa 500 kuhusu ushahidi unaowaonyesha majaji hao wakitaka kupewa hongo.
Majaji wengine 22 wa mahakama ya chini pia wamesimamishwa kazi huku wengine wakikana madai hayo.
Makala hayo ya bwana Anas yamelishtua taifa la Ghana na yameonyeshwa katika majumba ya kuonyeshea filamu katika mji mkuu wa Accra.
Saba hao ni majaji wenye nyadhfa za juu zaidi kusimamishwa kazi nchini humo.
Jaji mkuu Goergina Theodora Wood ameanzisha kesi dhidi yao kulingana na baraza la majaji nchini humo.
Uchunguzi pia utafanywa ili kubaini iwapo wana hatia au la.
Comments
Post a Comment