MBWA AMPIGA RISASI MMILIKI WAKE
Na katika kisa ambacho kimewaacha watu wengi kote duniani wamepigwa na butwaa,,,,
Mwanamke mmoja mmiliki wa mbwa huko Marekani alilazwa hospitalini baada ya jibwa lake kufyatua bastola na kumjeruhi mguu.
Amini usiamini ni tukio la kweli kabisa.
Afisa wa mazingira wa jimbo la, Indiana, Jonathon Boyd amenukuliwa akisema kuwa bi Allie Carter alikuwa ameenda kuwinda bata wa mwituni akiwa amejihami na bastola yake na jibwa lake.
''Baada ya muda akawa anahisi amechoka kisha akaweka bastola yake chini.''
''Kwa bahati mbaya jibwa hilo lilikanyaga bunduki hiyo na kufyatua risasi iliyomjeruhi bi Carter mguuni.''
Boyd anasema kuwa bibi huyo alijeruhiwa vidole vya mguuni lakini amepata matibabu.
Afisa huyo aliongezea kusema kuwa bi Carter hajakamilisha mafunzo ya msingi kabla hajaruhusiwa kuwa mwindaji na hivyo akasema huenda ajali hiyo ingeepukwa ikiwa angekuwa amekamilisha mafunzo hayo.
Ukistaajabu ya Musa ,,,,,,,
Toa maoni yako kuhusiana na tukio hilo la kipekee
Comments
Post a Comment