MPIGA PICHA AUWAWA PAMOJA NA FAMILIA YAKE
Mpiga picha wa runinga ya taifa nchini Burundi, pamoja na familia yake wameuawa katika mji mkuu Bujumbura.
Polisi mjini humo wanasema kuwa walikuwa wakijaribu kuwaokoa maafisa wenzao wa polisi waliokuwa wametekwa nyara.
Polisi
wanasema kuwa watu kumi waliuawa katika kisa hicho akiwemo mpiga picha
huyo wa runinga Christophe Nkeza-bahizi, mkewe na wanawe wawili pamoja
na afisa mmoja wa polisi.
Milio ya risasi na na milipuko ya mabomu yalisikika usiku kucha.
Ghasia
nchini Burundi, zilianza mwezi Aprili mwaka huu, baada ya Rais Pierre
Nkurunziza kutangaza angewania muhula wa tatu wa urais.
Katika
miezi ya hivi karibuni, Burundi imekumbwa na wimbi la mauaji ya kiholela
ya wanaharakati wa upinzani na maafisa wa usalama.
Haijajulikana mara moja ni nani aliyewateka nyara maafisa hao wa polisi
Comments
Post a Comment