DIAMOND AZIDI KUNYAKUWA TUZO
Msanii kutoka
bongo, Nasibu Abdul al maarufu '‘Diamond Platinumz'', amewabwaga wasanii
wengine wa Afrika na India na kuondoka na tuzo la onyesho bora yaani
Best African/Indian Act.
Hii ni kufuatia ushindani mkali
uliowavutia wasanii wengine kama vile Yemi Alade, AKA, Davido, DJ
Arafat, Indus Creed, Monica Dogra, Priyanka Chopra, The Ska Vengers,
Your Chin na Asia.
Diamond alikuwa jukwaani pamoja na wasanii
wengine tajika duniani akiwemo Justin Beiber ili kupokea tuzo hiyo
kwenye hafla iliyoandaliwa katika uwanja wa Mediolanum Forum mjini
Milan, Italia.
Mbali na Diamond, wasanii wengine walioshinda ni
Rihanna, aliyezawadiwa tuzo la mwanmuziki bora wa kike, Nicki Minaj
aliyetawazwa msanii bora wa muziki wa hip hop, huku wimbo wa Bad Blood
uliyoimbwa na Taylor Swift akishirikiana Kendrick Lamar ukituzwa kuwa
wimbo bora.
Msanii huyo ambaye anajulikana kama baba Tiffah
ameongeza idadi ya mataji aliyonyakua chini ya muda wa mwezi mmoja baada
ya kuondoka na tuzo tatu kwenye matuzo ya wanamuziki ya Afrimma ambapo
alinyakua mataji kadhaa kama vileo video bora ya densi, msanii bora wa
Afrika, na msanii bora wa Afrika Mashariki.
Comments
Post a Comment