MVULANA WA MIAKA 11 ADAIWA KUUA KWAJILI YA MBWA

LatashaImage copyrightWate 6 on your side
Image captionMamake Dyer anasema mvulana huyo alikuwa amezoea kumchokoza msichana huyo
Mvulana wa umri wa miaka 11 anazuiliwa katika jimbo la Tennessee nchini Marekani akituhumiwa kumuua msichana wa jirani baada ya mzozo kuhusu kitoto cha mbwa.
Mvulana huyo ameshtakiwa kwa kutekeleza mauaji.

Kwa mujibu wa polisi, mvulana huyo alimpiga risasi msichana huyo wa umri wa miaka minane Jumamosi jioni akitumia bunduki ya babake. Hii ni baada ya msichana huyo kumzuia kumuona mwanambwa wake.
Msichana huyo ametambuliwa kama McKayla Dyer. Mamake Latasha anasema watoto hao wawili wamekuwa wakienda shule moja.
“Alikuwa (mvulana huyo) amezoea kumtania, kumtusi na kumuonea. Aliacha kwa muda lakini ghafla jana alikuja na akampiga risasi,” Bi Dyer aliambia WATE-TV.
"Nataka msichana wangu anirudie," alisema.
Jirani yao Chastity Arwood aliambia WBIR News kuwa alisikia milio ya risasi na alipofika akamuona McKayla amelala kwenye nyasi.
Mvulana huyo anatarajiwa kufikishwa kortini Oktoba 28.
Shirika lisilo la kiserikali la Gun Violence Archive, ambalo hufuatilia visa vya ufyatulianaji wa risasi Marekani, linasema watoto 559 wa umri wa miaka 11 kwenda chini wameuawa au kujeruhiwa Marekani katika visa vya ufyatulianaji wa risasi mwaka huu.

Comments