NEC YAKATA MAJINA YA WATU MILIONI 1,031,769 KWENYE DAFTALI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA HUU

 
Watu milioni moja waondolewa kwenye daftari la wapiga kura Tanzania
Tume inayosimamia uchaguzi nchini Tanzania (NEC), imefuta majina ya wapiga kura zaidi ya milioni moja kutoka kwenye orodha ya watu waliojiandikisha kupiga kura.

Awali tume hiyo ilikuwa imetoa idadi ya wapiga kura milioni 23.7 waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu kupitia kwa mfumo wa kielektroniki (BVR).
Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema idadi hiyo imepigwa kalamu kufuatia shughuli ya kuhakiki majina ya watu wote waliojiandikisha.

 
Image caption Watu 181,452 walijiandikisha zaidi ya mara 
moja.
Majina ya watu milioni moja, 1,031,769 waliopatikana kuwa na makosa moja au zaidi yaliondolewa.
Jaji Lubuva alisema kuwa wengine waliojiandikisha zaidi ya mara moja, wengine hawakutimiza vigezo vya kuitwa Watanzania huku waliosalia wakiwa watu waliokosa sifa nyingine muhimu.
Kufuatia shughuli hiyo , Jaji Lubuva alisema wapiga kura watakaoruhusiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao watakuwa ni watu milioni 22,251,292.

 
 
Image caption Jaji Lubuva alisema wapiga kura watakaoruhusiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao watakuwa ni watu milioni 22,251,292.
Kisiwani Zanzibar wapiga kura wapatao laki 503,193 wataruhusiwa kushiriki uchaguzi mkuu tarehe 25.
Watu 181,452 walijiandikisha zaidi ya mara moja.
Wengine 845,944 waliandikishwa na wahudumu 74,502 waliokuwa kwenye mafunzo kabla ya kuanza shughuli kuu ya uandikishaji

 
Image caption Vituo vya kupigia kura 63,525 vitakuwa Tanzania bara huku Kisiwa cha Zanzibar kikitengewa vituo 1,580
Aidha majina ya watu 3,870 yalibainika kuwa watu waliokosa sifa za Mtanzania.
Wakati huohuo idadi ya vituo vya kupigia kura pia vimetangazwa.
Kutakuwa na vituo 65,105 vya kupigia kura katika uchaguzi ujao.
Vituo vya kupigia kura 63,525 vitakuwa Tanzania bara huku Kisiwa cha Zanzibar kikitengewa vituo 1,580 vya kupigia kura.

Comments