ODOM AKUTWA AKIWA AMEZIRAI KWENYE DANGURO
Aliyekuwa mchezaji
wa mpira wa vikapu nchini Marekani Lamar Odom anatibiwa hospitalini
baada ya kupatikana amezirai katika danguro mjini Nevada ,kulingana na
mamlaka.
Maafisa wa polisi waliitwa katika danguro la Love Ranch
huko Crystal mjini Nevada baada ya kupatikana akiwa hana fahamu siku ya
jumanne.
M'marekani huyo alibebwa na gari na kupelekwa hadi hospitalini kwa kuwa alikuwa mrefu mno kubebwa katika ndege.
Bwana Odom mwenye umri wa miaka 35 amezichezea Miami,Dallas na Los Angeles Lakers pamoja na Clippers.
Pia aliichezea Marekani katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2004 na kushinda medali ya shaba.
Ugonjwa wake haujulikani lakini wasamaria wema walituma ujumbe wao kwa mtandao wa twitter baada ya habari hizo kusambaa.
Bwana Odom ambaye alikuwa amemuoa nyota wa kipindi
cha Keeping up with the Kardashians, Khloe Kardashian amekuwa mnywaji
mkubwa wa pombe na dawa za kulevya.
Alihusishwa na kuendesha gari
akiwa mlevi mwaka 2013 na kupigwa marufuku katika shirikisho la mchezo
wa mpira wa vikapu nchini Marekani NBA kwa kukiuka sheria dhidi ya dawa
za kulevya ya mwaka 2000.
Odom na Kardashian waliowana mwaka 2009 katika sherehe ambayo ilionyeshwa katika kipindi cha runinga ya Marekani E.
Walitalakiana
mwaka 2013.Odom alishinda ubingwa wa NBA akiwa na klabu ya Lakers mwaka
2009 na 2010 na alitajwa kuwa mchezaji wa sita bora mwaka 2011.
Mara ya mwisho kucheza katika NBA ni mwaka 2013 alipokuwa akiichezea Clippers.
Comments
Post a Comment