RONALDO AWEKA REKODI NA KIATU CHA NNE CHA DHAHABU,ASEMA ANATAKA KUSTAFU AKIWA MADRID




Mshambuliaji wa Real Madrid amekabidhiwa kiatu chake cha nne cha dhahabu na kuweka rekodi mpya.

Kiatu hicho cha dhahabu hutolewa kwa mfungaji bora wa ligi moja ya Ulaya ambaye amefunga mabao mengi zaidi kuliko ligi zote za Ulaya.
 

Ronaldo ambaye ametangaza anataka kustaafu soka akiwa Real Madrid amesema angependa kushinda makombe zaidi.
“Nimesema kila mara, nataka kushinda zaidi. Hapa nina miaka 30, nina uwezo wa kushinda zaidi na zaidi.
“Ninaamini nina miaka mitano au sita ya kucheza zaidi,” alisema.

Comments