SERIKALI IMEKEMEA VIKALI TAARIFA ZINAZOZUSHWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI

Cloudsfm Radio's photo.
Baada ya kusambaa kwa habari kwenye mitandao ya kijamii kuzusha taarifa ya kifo cha Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda, na kuna chombo cha habari.
kimeandika vitu ambavyo si kweli katika uteuzi aliyoufanya Mh. Rais Jakaya Kikwete siku chache zilizopita kwa kuwa teuwa wakuu wa Wilaya. Msemaji mkuu wa Serikali pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene ameongea na waandishi wa Habari leo juu ya uzushi huo.
“ Nimewaiteni waandishi wa habari nataka kuzungumzia taarifa ya uteuzi aliyoufanya Mh. Rais siku chache zilizopita, na kuna baadhi ya vyombo vya habari wameeleza mambo matatu katika uteuzi ule moja wameaandika rais analipa fadhira, sehemu ingine wanasema ufujaji wa fedha za serikali na tatu wameandika amewapa maswaiba wake ambao walikosa nafasi katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi, hayo yote ni mamlaka ya Mh. Rais kuteua kwa kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kingine hakuna kigezo chochote kati ya chombo hicho cha habari kilichoandika na kumfanya Mh. Rais asiteu watumishi, kumbuka tuna Wilaya na zote zinahitaji nafasi zijazwe na Watumishi wa Umma, suala la kusema maswaiba si la kweli labda kuwe kati ya wale walioteuliwa itokee kwa mtu ni raia wa kigeni ndio unaweza kusema rais amepotoka kwa kumteuwa mtu baki na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Pia kuna taarifa zinazoandikwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuzusha kwa taarifa ya Dkt. Kigoda kuwa amefariki hizo taarifa hazina ukweli ila bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Apolo nchini India.
Mimi ndio msemaji mkuu wa serikali ninapo kaa na kusema kumzushia mtu taarifa za kifo si jambo jema, na taarifa zingine cha David Mwamnyange kuwa amelishwa sumu hizo taarifa si sahihi na serikali inafanya uchunguzi kuhusu matukio hayo yote na wote waliohusika kuweka hizo taarifa serikali ikiwabaini tutawatangaza wahusika ni nani na hatua zitachukuliwa.
Naomba niwaombe wengine mna blogs, Facebook zenu naomba usi-post kitu kabla hujahakikisha ni habari ya ukweli.” Assah Mwambene

Comments