VITAMBULISHO 134 VYA KUPIGIA KURA VYAKAMATWA KAGERA
Vitambulisho 134 vya Kupigia kura, vimekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa –TAKUKURU- mkoani Kagera baada ya kukutwa vimenunuliwa na Kundi la watu kutoka kwa wapiga kura.
Taarifa ambazo zimethibitishwa na Naibu mkuu wa
Takukuru mkoani Kagera, John Joseph vitambulisho hivyo vimekamatwa vikiwa tayari
vimenunuliwa kutoka kwa wananchi kwa bei ya kati ya shilingi 5,000 hadi
10,000.
Amesema kuwa kukamatwa kwa Vitambulisho hivyo,
kumetokana na baadhi ya Vijana walioshawishiwa kuuza kadi hizo na kundi la watu
wanaopita, kutoafiki na kisha kulazimishwa kufanya hivyo.
Comments
Post a Comment