WANANCHI WASIKITISHWA NA KIFO CHA ALIYEKUWA WAZIRI DK.ABDALLAH KIGODA

Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda amefariki dunia juzi saa 10 jioni nchini India alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Wananchi wameeleza kusikitiswa kwao juu ya kifo cha aliyekuwa waziri wa viwanda na biashara dk. kigoda aliyefariki octobar 12 huku nchini India alikokuwa amepelekwa kutibiwa mkazi mmoja wa makete anayejulikana kwa jina la Edna ndelwa ameeleza kusikitishwa kwake juu ya kifo cha kiongozi huyo na kusema ni pigo kubwa kwa familia ya marehemu na nchi kwa ujumla na pia aliwaomba wananchi pamoja na familia ya marehemu kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha masikitiko ya taarifa hiyo ya kifo iliyo sibitishwa na 
 
Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila juu ya taarifa hizo, na kusema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

Kwa mujibu wa kaka wa marehem Sadiki Kigoda aliyezungumza na vyombo vya habari siku chache zilizopita, alisema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo kushindwa kufanya kazi.

Comments