WASIMAMIZI WAWILI WA UCHAGUZI WA JERUHIWA VIBAYA BAADA YAKUKAMATWA NA KURA FEKI
Wasimamizi wasaidizi watatu wamejeruhiwa kwa kipigo kutoka kwa
wananchi waliowashuku kusafirisha masanduku yenye kura
zilizokwishapigwa usiku wa kuamkia jana.
Tukio
hilo liliwalazimu polisi kupiga mabomu ya machozi mfululizo kwa nyakati
tofauti kati ya saa 5:00 na saa 8:00 usiku wa kuamkia jana ili
kuwatawanya wananchi waliofurika kituo cha Polisi Himo.
Tafrani
hiyo iliibuka baada ya wasimamizi hao wasaidizi kukamatwa na wananchi
kati ya eneo la Marangu Kilema na mji mdogo wa Himo wakiwa na gari
linalodaiwa ni la kada wa CCM.
Baada
ya kukamatwa na masanduku hayo ya kura yakiwa na karatasi ambazo
hazijapigwa bado, wananchi hao waliwatembezea mkong’oto wasimamizi hao
na baadhi kujeruhiwa vibaya.
Kamanda
wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema kuwa wasimamizi
hao walipigwa na wananchi baada ya kushukiwa kusafirisha masanduku ya
kura ambayo yana kura zilizokwisha pigwa.
“Baada
ya hao wasimamizi kukamatwa walipelekwa kituo cha Polisi Himo na
taarifa zilizozagaa zilivuta wananchi wengi waliofurika kwenye hicho
kituo,”alisema Kamanda Ngonyani.
Kamanda
Ngonyani alisema polisi waliwataka wananchi hao kutawanyika lakini
wakawa wanagoma na kuanzisha vurugu hali iliyowalazimu polisi kutumia
nguvu ya ziada kuwatawanya.
Kituoni
hapo alikuwepo pia mgombea Ubunge Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP,
Agustino Mrema na hasimu wake mkubwa ambaye naye anagombea kwa tiketi ya
NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Hata
hivyo kamanda huyo alisema, baada ya kutokea kwa tafrani hiyo
waliwasiliana na msimamizi wa uchaguzi, Fulgence Mponji ambaye baada ya
kufika kituoni aliwatambua ni watumishi wa Tume.
Taarifa
zaidi zinasema baada ya wasimamizi hao kufikishwa kituo cha polisi,
wananchi walifunga barabara zote zinazoingia katika mji mdogo wa Himo
huku wakikagua kila gari linalopita.
Madereva
wa magari ambao walikaidi kusimama na kukaguliwa, walijikuta matatani
kwa magari yao kuvunjwa vioo kwa kutumia mawe hali iliyowalazimu Polisi
kutumia mabomu kuwatawanya.
Mrema
alipotafutwa kuzungumzia hali hiyo, alisema asingeweza kusema chochote
kuhusu uhalali wa karatasi hizo za kura kwani alimkabidhi jukumu hilo
kijana wake ambaye alikuwa hajampata.
“Tukiwa
pale polisi tuliambiwa kila mmoja ateue mtu atakayeshiriki kuzihakiki
pamoja na msimamizi. Kuna kijana wangu nilimpa hiyo kazi mpaka sasa bado
sijakutana naye anipe mrejesho,”alisema.
Kwa
upande wake, Mbatia aliilaumu NEC kwa kutaka kuvuruga uchaguzi huo kwa
kuwapa wasimamizi vifaa nyeti vya uchaguzi kuvisafirisha bila ulinzi wa
Askari polisi au Mgambo.
Comments
Post a Comment