BAADA YA KUSHINDA UDIWANI SASA BABA LEVO KUTUMIA MILION 110 KUTENGENEZA STUDIO KALI
Baba Levo ambaye hivi sasa ni mheshimiwa Diwani Mteule wa Kata ya Mwanga, Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT –Wazalendo, amepanga kubadili mazingira ya muziki Kigoma na kuwavuta wasanii wa Dar es Salaam katika mji huo kupitia uwekezaji wa zaidi ya milioni 110.
Msanii
huyo wa Bongo Flava ameeleza kuwa baada ya kushinda udiwani, amepanga
kutekeleza ahadi yake ya kuanzisha studio kubwa ya muziki zaidi ya
studio zote zilizopo Dar es Salaam, uwekezaji utakaomgharimu kiasi hicho
cha fedha.
“Inafunguliwa
studio ambayo ni kubwa nadhani kushinda hata studio zote za Dar es
Salaam lakini inafunguliwa Kigoma. Studio hiyo gharama yake ni kama
milioni 110 hivi,” ameiambia The Chart ya 100.5 Times Fm.
Amesema
kuwa lengo la kufungua studio hiyo ni utekelezaji wa sera za chama
chake na wazo lake katika kukuza vipaji vya sanaa ya muziki na uigizaji
na kwamba anataka wasanii kutoka nje ya nchi pamoja na Dar es Salaam
wawe wanafunga safari kuelekea Kigoma Mjini kurekodi nyimbo zao.
Akizungumzia
ushindi wa Udiwani alioupata, Baba Levo ameeleza kuwa ushindi huo kwake
ni muhimu sana kwani alichagua kata iliyokuwa na ushindani mkubwa
iliyokuwa mikononi mwa CCM kwa miaka 14.
Comments
Post a Comment