ENDELEA KUPIGA KULA ZA KUCHAGUA MCHEZAJI BORA WA AFRICA KUPITIA BBC SWAHILI
Wagombea watano wa
tuzo ya BBC kwa mwanasoka bora wa mwaka 2015 wametangazwa kwenye hafla
maalum iliyoandaliwa mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mshindi wa tuzo la mwaka 2014 Yacine Brahimi, yupo kwenye orodha hiyo pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang, André Ayew, kutoka Ghana, Sadio Mané na Yaya wote wa Ivory Coast.
Mshindi ataamuliwa na mashabiki wa soka Afrika ambao watapewa fursa kupiga kura hadi tarehe 30, Novemba.
Unaweza kupiga kura mtandaoni kwa kubofya hapa au kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu kwa nambari +44 7786 20 20 08:
- Ujumbe 1 kwa-Emerick Aubameyang
- Ujumbe 2 kwa André Ayew
- Ujumbe 3 kwa Yacine Brahimi
- Ujumbe 4 kwa Sadio Mané
- Ujumbe 5 kwa Yaya Touré
Mshindi atatangazwa ijumaa tarehe 11 mwezi December wakati wa matangazo maalum kwenye BBC World News na BBC World Service, wakati mitandao ya BBC Sport na BBC Africa ikitoa pia matangazo. Kwa sheria na masharti bofya hapa.
Wagombea wa tatu mwaka huu waliopigiwa kura na wanahabari 46 kutoka Afrika wamewahi kushinda tuzo hilo: Ayew (2011), Touré (2013) na Brahimi (2014).
Aubameyang ameorodheshwa kwa mwaka wa tatu mfululizo wakati Mané akijumuishwa kwa mara ya kwanza.
Mshambulizi Aubameyang amenawiri katika ufungaji magoli mwaka huu, akimaliza kama mfungaji mabao bora wa Borussia Dortmund msimu uliopita kabla ya kuandikisha rekodi mpya ujerumani kati ya 2015-16.
Mwezi Oktoba raia huyo wa Gabon, mwenye umri wa miaka 26,alikuwa mtu wa kwanza kufunga bao katika mechi nane za mwanzo katika Bundesliga huku mechi zake 17 za mashindani zikiishia ushindi mkubwa wa mabao 20 .
Mwaka huu pia umeshuhudia mafanikio makubwa kwa Ayew na ingawa haikuwa kilele, kombe la mataifa barani Afrika yalipunguza machozi yake huku the Black Stars ikishindwa na Ivory Coast.
Alikuwa na ushawishi mkubwa katika kampeni ya Ghana na kisha kuuhamisha ufanisi wake katika ligi guu ambako alifunga mabao matano katika mechi kumi alizochezea Swansea City.
Brahimi anayeichezea FC Porto amekuwa mchezaji anayelengwa barani Afrika na ulaya lakini raia huyo wa Algeria, 25, amekuwa akiongeza mabao katika ufanisi wake kwa kufunga jumla ya magoli 13 msimu uliopita huku akiisaidia klabu yake kushiriki robo fainali za ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita
Mojawepo wa mafanikio yake makubwa yalikuwa katika shindano hilo msimu uliopita ambako chenga chenga zake zingefananishwa tu na Eden Hazard wa Chelsea au nyota wa Barcelona Lionel Messi.
Tarehe 16 Mei, Mane anayeichezea Southampton alihitaji tu sekunde 176 kufunga hattrick ya haraka zaidi katika hisoria yake ya kucheza katika Premier League.
Ni miongoni mwa mabao yake 10 katika mechi 29 za Ligi ya Premia mwaka huu, matokeo yaliyoimarishwa zaidi hasa ikizingatiwa yeye ni mchezaji wa kiungo cha kati.
Mchezaji wa pekee katika orodha hii aliyewahi kunyakuwa kombe ni Touré na ilikuwa zawadi kubwa iliyoje wakati alipoiongoza Ivory Coast kunyakuwa taji la kwanza katika michuano ya kombe la mataifa katika kipindi cha zaidi ya miongo miwili.
Akiwa ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwaliko wapinzani wake, mchezaji huyo wa kiungo cha kati ni mhimili katika matumaini ya klabu ya Manchester City kunyakuwa mataji na kazi yake imetambuliwa na Fifa ambayo imemteuwa kama mchezaji wa pekee kutoka Afrika kuania taji la kifahari la Ballon d’Or.
Comments
Post a Comment