UFARANSA YAWAUA WAPIGANAJI 32 SYRIA

 
wapiganaji wa islamic state mjini Raqqa
Mashambulio ya Ufaransa na mataifa mengine dhidi ya ngome ya Islamic State huko Raqqa nchini Syria siku ya jumapili yamewauwa takriban wapiganaji 33,wanaharakati wamesema.

Kundi la wapiganaji wa haki za kibinaadamu kutoka Syria limesema kuwa wengi walifariki wakati vituo vya kukagua watu vilivyoshambuliwa.
 
Ndege za kijeshi za Ufaransa zashambulia mji wa Raqqa
Pia limeripoti kwamba familia za viongozi wa Islamic State zimeanza kuondoka Raqqa na kuelekea katika ngome nyengine ya kundi hilo katika mji wa Iraq wa Mosul.
Hatahivyo chombo kimoja cha habari kinachohusishwa na IS kimesema kuwa hakuna majeraha yoyote yaliotekelezwa na mashambulio hayo.
 
Wapiganaji wa islamic state
Kituo hicho cha Aqama kilisema siku ya jumatatu na jumanne kwamba ndege za Ufaransa zililenga ''maeneo yasio na watu,huku kundi hilo likidai kuwa lina ulinzi wa kutosha''
Kundi hilo la haki za kibinaadamu nchini Syria ambalo lina wanahabari wake nchini humo,limesema kuwa wapiganaji 33 waliaminika kuuawa katika mashambulio hayo,lakini miili yao iliharibiwa vibaya hali ya kuwa haiwezi kutambulika na hivyobasi haliwezi kutoa idadi sawa ya waliouwawa.

Comments