VIONGOZI WALIOISALITI CCM KWENYE UCHAGUZI MKUU HUKO TABORA WASIMAMISWA KAZI
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tabora Mjini, kimewasimamisha viongozi wanne wa Kata ya Chemchem kwa kukisaliti chama hicho katika mchakato uliopita wa kura za maoni hadi Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 Mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Katibu wa chama hicho, Kanuth Ndaghine
alisema sababu za kuwasimamisha viongozi hao ni kukisaliti chama na
kutosimamia kikamilifu uchaguzi katika ngazi za udiwani wa kata hiyo.
Ndaghine
alisema viongozi hao walikuwa hawakisaidii chama kupata ushindi bali
waliegemea chama pinzani ambacho kiliweza kuchukua nafasi ya udiwani
kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika kata ya Chemchem mkoani Tabora.
Aidha
alisema wanachama na wananchi hawana imani na viongozi hao tangu
kipindi cha mchakato wa kura za maoni mpaka kufikia uchaguzi mkuu.
Hata hivyo, alieleza kusikitikia kitendo kilichofanywa na viongozi hao cha kukisaliti chama kwa kuwa walikuwa na wagombea wao katika mchakato wa kura za maoni ambao kura hazikutosha.
Hata hivyo, alieleza kusikitikia kitendo kilichofanywa na viongozi hao cha kukisaliti chama kwa kuwa walikuwa na wagombea wao katika mchakato wa kura za maoni ambao kura hazikutosha.
Aliyeshinda
ni Elizabert Shoki aliyepata kura nyingi zilizopigwa na wanachama wa
CCM katika kata hiyo. Viongozi hao walishindwa kumuunga mkono aliyekuwa
mgombea wa chama hicho na kukipigia kura CUF, kitu ambacho hakikubaliki
katika chama kwa kuwa wao ni viongozi wa kata hiyo.
Pamoja
na CCM kukosa kata hiyo, alisema katibu huyo kuwa viongozi hao hawafai
katika chama kwa sababu wanaonekana dhahiri kukisaliti chama hicho na
kuwatia aibu wanachama na wananchi kwa ujumla.
Aliwataja
viongozi waliosimamishwa uongozi kuwa ni Mwenyekiti wa Kata Juma
Mapunda, Katibu Kata Mwajuma Boko, Katibu wa siasa na Uenezi kata hiyo
Issa Water na Katibu uchumi na fedha, John Muhando.
Kwa
upande wake Katibu wa Siasa na Itikadi, Uenezi Wilaya ya Tabora Mjini,
Rashidi Tollu alisema waliwateua viongozi wengine ili kukaimu nafasi
hizo za viongozi waliosimamishwa na kuweka wengine.
Waliowekwa
ni Kisuzi Mswanyama Mwenyekiti, Tatu Balola Katibu kata, Hussenu Sengo
katibu wa Siasa na Uenezi wa kata Selemani Mzee Kaimu katibu wa Uchumi
na fedha. Tollu amewataka viongozi hao waliokaimishwa nafasi hizo
wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa kwa wanachama na wananchi wote kwa
ujumla, kwani wananchi wana imani na chama hicho ambacho kinasimamia
misingi Imara ya amani,umoja na upendo.
Akizungumzia
kusimamishwa kwao, Juma Mapunda alisema hawawezi kuzungumza chochote
juu ya kusimamishwa kwao isipokuwa wanaandika barua ili waipeleke kwa
Mwenyekiti wa chama hicho, Abdulrahman Nkonkota.
Comments
Post a Comment