MUUAJI AJIITA SHUJAA COLORADO
Mwanamume mmoja
aliyeua watu watatu katika shambulio katika kliniki ya matibabu nchini
Marekani katika jimbo la Colorado mwezi uliopita amekiri makosa.
Robert Dear aliingilia mfumo wa kisheria wa mahakama na kutangaza kwamba yeye ni mshindi kwa ajili ya watoto.aliwashutuma waendeshaji wa cliniki hiyo katika masuala ya uzazi wa mpango na kuua watoto.
Shirika hilo la uzazi wa mpango lenye kuendesha shughuli zake nchi nzima ya Marekani limejikuta katika mjadala mzito wa kisiasa juu ya masuala utoaji mimba kutokana na mazoezi yake yenye utata la kutoa mimba changa kwa ajili ya utafiti
Comments
Post a Comment