EXCLUSIVE >> KOLO TOURE AMESAJILIWA NA CELTIC KWA MWAKA MMOJA

Headlines za usajili leo July 24 2016 zinamuhusu beki wa kati wa kimataifa wa Ivory Coast aliyewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal, Man City na Liverpool Kolo Toure, jina la beki huyo leo limetangazwa kusajiliwa na klabu ya Celtic ya Scotland.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 35 ametangazwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja, hivyo hiyo itakuwa ni mara  ya pili kwa Kolo Toure kufundishwa tena na kocha Brendan Rodgers ambaye amewahi kumfundisha katika kikosi cha Liverpool.
573143905b4ecb23fced3fafe53f93d4 (1)
Toure akiwa katika ardhi ya England amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu na mataji matatu ya Kombe la FA “Toure nimemleta kwenye kikosi hichi cha vijana najua atawasaidia vijana na kuwa kiongozi mzuri kama ilivyo kwa Scott Brown ambaye amekuwa ni kiongozi mzuri katika timu” >>> Brendan Rodgers

Comments