KIKOSI CHA RIADHA CHA URUSI CHANUSULIKA MARUFUKU

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki imeamua kutokipiga marufuku kikosi chote cha Urusi kutoka kwa mashindani ya Rio, baada ya uchunguzi kubainisha kuwa wanariadha wa urusi walikuwa wamesaidiwa na serikali kutumia madawa yanayotutumua misuli.


 
IOC ilisema kwa mashirika ya kimataifa yanayosimaia michezo tofauti yanastahili kuchukua hatua kwa kila mwanariadha.
Hii inamaanisha kuwa mwanariadha yeyote wa Ursui ambaye atakubalika atafanyiwa uchunguzi zaidi.
Hata hivyo hakuna mwanariadha yeyote wa Urusi ambaye amekumbwa na kashfa hiyo awali ataruhusiwa kushiriki mashindano ya Rio yanayofanyika chini ya wiki mbili zinazokuja

Comments