LYON YAKATAA OMBI LA ARSENAL KUMNUNUA LACAZETTE
Klabu ya Lyon imekataa ombi la Euro milioni 35 kutoka Arsenal kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 25 alifunga mabao 21 katika mechi 34 msimu uliopita na kandarasi yake katika klabu hiyo inakamilika 2019.
Katika taarifa yake katika mtandao wa Twitter,Klabu hiyo ya Ufaransa ilisema Lacazette hanunuliki na ni miongoni mwa viongozi wa timu hiyo ya kocha Bruno Genesio.
Lyon ilikana ripoti ya gazeti moja kwamba ilikataa ombi la Euro milioni 48 kutoka kwa klabu hiyo ya Uingereza.
Comments
Post a Comment