Aliye jifanya Ofisa usalama feki afungwa jera huyu hapa
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemhukumu Seleman Manoti, kifungo cha
miaka miwili jela kwa kupatikana na hatia ya kujifanya usalama wa Taifa.
Hata hivyo, mahakama imetoa hukumu hiyo bila mshitakiwa kuwepo
mahakamani kutokana na kuruka dhamana kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa.
Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Flora Haule alisema kuwa
upande wa mashitaka, ulileta mashahidi wanne kwa ajili ya kuthibitisha
tuhuma hizo.
Alisema kutokana na ushahidi uliotolewa, mahakama imeridhishwa na
ushahidi huo na kwamba mahakama inamtia hatiani mshitakiwa licha ya yeye
kutokuwepo.
“Hati ya kumkamata mshitakiwa itolewe na adhabu hii itaanza kutumika
pindi mshitakiwa atakapokamatwa kwani alitoroka akiwa na haki ya
kusikilizwa,” alisema Hakimu Haule.
Wakili wa Serikali, Ester Kyara aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa iwe fundisho kwa wengine.
Inadaiwa kuwa Novemba 19, 2014 maeneo ya Kariakoo Msimbazi wilayani
Ilala, mshitakiwa alijitambulisha kwa Issaya Odelo na Charles Odinga
kuwa Ofisa Usalama wa Taifa, kitu ambacho alijua si kweli. Katika hatua
nyingine, kondakta Ally Salum (23), mkazi wa Mwananyamala, amehukumiwa
kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kuiba
daladala.
Mbali na mshitakiwa huyo, Exavery Kaunga (44) ambaye ni mlinzi na
mkazi wa Kiwalani, Minazi Mirefu, aliachiwa baada ya ushahidi dhidi yake
kuwa na shaka.
Akitoa hukumu hiyo jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Hakimu
Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan, alisema kuwa upande wa mashitaka ulileta
mashahidi wanne kuthibitisha kosa hilo
Comments
Post a Comment