Apigwa na panga kichwa adi kufa ma kaka yake tumbo moja
MKAZI wa kijiji cha Ntalamila kata ya Miyula wilayani Nkasi mkoani
Rukwa, Baraka Kaengele (23) ameuawa kikatili na kaka yake wa tumbo moja,
Edward Kaengele (25) kwa kumshambulia na kumpasua kichwa kwa panga na
ubongo kutokeza nje.
Inadaiwa wanandugu hao walihitilafiana wakati wakigawana fedha, walizolipwa baada ya kumaliza kufanya kazi za vibarua shambani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alidai tukio hilo
lilitokea Oktoba 27, mwaka huu saa mbili na nusu usiku katika kijiji cha
Ntalamila kilichopo kata ya Miyula, wilayani Nkasi.
“Chanzo cha mauaji ni ugomvi wa kifamilia ambapo ndugu hawa wa
familia moja walikuwa wakigombania fedha walizolipwa baada ya kufanya
kazi za vibarua katika mashamba,” alieleza Kamanda Kyando
Comments
Post a Comment