Arsenal yazidi kutamba EPL yaichabanga sunderland 4-1
Sanchez alifungua ukurasa wa mabao kwa Arsenal kwa goli safi la
kichwa baada ya kumzidi ujanja beki wa Sunderland Lamine Kone kufuatia
krosi nzuri ya Oxlade-Chamberlain
Arsenal walinyimwa penati ya wazi baada ya Sanchez kuangushwa ndani
ya eneo la penati kabla ya mshambuliaji wa Sunderland Jermain Defoe
kusawazisha bao kwa penati baada ya kipa Petr Cech kumwangusha Duncan
Watmore.
Hata hivyo baada ya dakika sita tu na sekunde 20 Arsenal tayari
walikuwa mbele kwa mabao 3-1 kufuatia magoli mawili ya Olivier Giroud
aliyeingia kutoka benchi.
Baadaye Sanchez alimalizia goli la nne na kuzidisha maafaa kwa Sunderland
Ushindi wa leo umewabakisha Arsenal nafasi ya pili kwenye msimamo wa
ligi nyuma ya Manchester City wote wakiwa na jumla ya alama 20 lakini
wakizidiana tofauti ya mabao.
Comments
Post a Comment