Askofu Gwajima apelekewa bastola hospitali
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa washtakiwa watatu
walipeleka bastola kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat
Gwajima wakati amelazwa katika Hospitali ya TMJ baada kubaini
wanaihifadhi kinyume cha sheria.
Ofisa Upelelezi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Sajini Abogasti (46) alidai hayo jana wakati akitoa
ushahidi katika kesi ya kushindwa kuhifadhi silaha inayomkabili Gwajima
na wenzake Yekonia Bihagaze, George Mzava na Geoffrey Milulu.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shedrack Kimaro kutoa
ushahidi wake, Sajini Abogasti alidai kuwa Bihagaze, Mzava na Milulu,
walipeleka silaha kwa Gwajima wakati akiwa amelazwa katika Hospitali ya
TMJ.
Alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa Mkuu wa Upelelezi
Kinondoni alimuunganisha na Mkuu wa Kituo Kawe, Pamphil ambaye
alimkabidhi begi lililokuwa na bastola namba CAT 5802, risasi tatu
zilizokuwa katika kasha lake (magazine), CD mbili, risasi 17 za bastola
na kitabu cha umiliki silaha, chupi na hati ya kusafiria ya mchungaji
huy
Comments
Post a Comment