Breaking News: Bondia Thomas Mashali auwawa, mwili wake waokotwa vichakani Dar

Tokeo la picha la thomasi mashali

Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali, hatunaye.Taarifa zinaeleza ameuwawa kwa kupigwa maeneo mbali mbali ya mwili na baadaye 
kuokotwa na wananchi walio itambua sura yake taarifa zinasema  marehemu thomas mashari aliokotwa
vichakani maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.

Yassin Abdallah maarufu kama Ustaadhi, mmoja wa viongozi wakongwe wa mchezo wa ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

"Tumethibitishiwa hizo taarifa za majonzi kabisa, mwili upo Muhimbili na msiba upo kwao Tandale," alisema Ustaadhi

Comments