DROO YA EFL HII HAPA MAN UNTED VS WEST HAM

EFL-CUP-2016-17DROO ya Mechi za Robo Fainali ya EFL CUP, Kombe la Ligi la England, imefanyika hii Leo mara baada ya Mechi ya mwisho ya Raundi ya 4 ambayo Man United iliwabwaga Mabingwa Watetezi wa Kombe hili Man City 1-0 huko Old Trafford.
Katika Droo hiyo, Vigogo wote wa Ligi Kuu England waliobakia kwenye Mashindano haya wamepangwa kucheza Mechi zao Viwanja vya Nyumbani kwao na hiyo ni faida kubwa kwao.
DROO KAMILI:

Arsenal v Southampton
Hull City v Newcastle
Man United v West Ham
Liverpool v Leeds United
+++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Msimu huu hili Kombe la Ligi halina Mdhamini na limebatizwa English Football League Cup, EFL CUP.
-Huko nyuma Kombe la Ligi, kwa sababu za kiudhamini, liliwahi kubatizwa Coca-Cola Cup, Worthington Cup, Carling Cup na Capital One Cup.
+++++++++++++++++++++++++
Mechi za Robo Fainali zitachezwa Wiki ya kuanzia Novemba 28.
EFL CUP
Matokeo:
Raundi ya 4
Jumanne Oktoba 25
Arsenal 2 Reading 0         
Bristol City 1 Hull 2          
Leeds 1 Norwich 1 [2-2 baada Dakika 120, Leeds Penati 3-2]         
Liverpool 2 Tottenham 1             
Newcastle 6 Preston 0
Jumatano Oktoba 26
Southampton 1 Sunderland 0               
West Ham 2 Chelsea 1               
Man United 1 Man City 0

Comments