FARID MUSSA SASA MAMBO SAFIIIIII NJIA NYEUPE KWENDA HISPANIA
Wakati wasiwasi ukiwa umetanda kwamba huenda ndoto za Farid Musa
kucheza soka la kulipwa Ulaya zikawa zimefifia, sasa kuna habari njema
kwamba kiungo huyo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania
‘Taifa
Stars huenda akasafiri kwenda kujiunga na timu yake ya Tenerife
inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Hispania.
Awali suala la Farid kuendelea kuonekana Tanzania huku akiwa amefuzu
majaribio kwenye klabu ya Tenerife lilizua mijadala hadi kupelekea
nahodha wa timu ya taifa Mbwana Samatta kuhoji nini kimefichika nyuma ya
pazia juu ya Farid kujiunga na timu yake ambapo tayari alishafuzu
majaribio.
General Manager wa Azam FC, Abdul Mohamed amethibitisha kukamilika
kwa kibali ambacho kitamruhusu Farid kufanya kazi nchini Hispania na
ameahidi kuwa, klabu inafanya jitihada kuhakikisha Farid anaondoka
mapema kwenda kujiunga na klabu yake ya Tenerife.
“Kibali chake cha kazi kimetoka siku moja ama mbili zilizopita,
sasahivi tunasubiri kukamilika kwa baadhi ya taratibu na punde Farid
ataelekea nchini Hispania kwenye timu ya Tenerife kwa ajili ya kuanza
maisha yake mapya,” amethibitisha Abdul Mohamed.
“ITC ya Farid imetumwa muda mrefu sana ipo Tenerife masuala ya ITC na
makubaliano kati ya klabu na klabu tulishamaliza kilichokuwa
kinasubiriwa ni kibali cha kazi kutoka ili kwenda kufanya kazi.”
“Tunaamini punde Farid ataanza safari yake, tunajitahidi hadi kufikia mwisho wa mwezi huu kila jambo liwe limekamilika.”
Comments
Post a Comment