HIGUAIN AISALITI NAPOLI APIGA BAO JUVENTUS IKISHINDA 2_1

Gonzalo Higuain Jana alufunga Bao la ushindi kwa Juventus dhidi ya
Klabu yake ya zamani Napoli kwenye Mechi ya Ligi Serie A huko Italy.
Bao hilo lilikuja Dakika ya 71 kwenye Mechi iliyochezwa huko
Juventus Arena Jijini Turin na kuwapaisha Mabingwa Watetezi Juve
kileleni mwa Serie A wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili AS Roma.
Juve sasa wana Pointi 27 kwa Mechi 11, AS Roma Pointi 22 kwa Mechi
10 na kufuatia Napoli wenye 20 kwa Mechi 11 na AC Milan ni wa 4 wakiwa
na Pointi 19 kwa Mechi 10.
Jana Juve walitangulia kwa Bao la Dakika ya 50 la Leonardo Bonucci na Napoli kurudisha Dakika ya 54 kupitia Jose Callejon.
Lakini Shujaa akawa Higuain katika Dakika ya 71 kwa Shuti ambalo lilimzidi Kipa Pepe Reina.
Comments
Post a Comment