JK atoa onyoo kali mtandaoni kuhusu matumizi ya picha zake
Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya
Kikwete amelalamika kutokana na kile alichosema ni kutumiwa vibaya kwa
picha zake mtandaoni na 'kulishwa maneno'.
Takriban mwaka mmoja tangu astaafu, Bw Kikwete, rais wa awamu ya nne, amesema anafaa kuruhusiwa apumzike.
Aidha, amesema anamuunga mkono Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli, pamoja na serikali yake.
"Nimestaafu
naomba niachwe nipumzike. Nisingependwa kuhusishwa na siasa za
mtandaoni dhidi ya Serikali. Namuunga mkono Rais na Serikali yake,"
ameandika kwenye Twitter.
"Nasikitishwa sana na matumizi mabaya ya
picha zangu mtandaoni hususan watu kunilisha maneno kwa kutaka kutimiza
malengo yao ya kisiasa."
chanzo;bbc swahili.>>>kakwaya100
Comments
Post a Comment