KIKOSI KAMILI CHA YANGA LEO DHIDI YA MBAO FC TAMBWE KAANZA

BAADA
ya kutokea benchi Jumatano na kufunga mabao mawili, Yanga ikishinda 4-0
dhidi ya JKT Ruvu, mshambuliaji Mrundi Amissi Joselyn Tambwe leo
ameanzishwa dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.
mfululizo wa Ligi Kuuya Vodacom Tanzania Bara ikitoka kushinda 4-0
Jumatano dhidi ya JKT Ruvu, mabao mengine yakifungwa na Simon Msuva na
Obrey Chirwa.
Na
Tambwe hajaanza tangu Jumatano ya Oktoba 12 Yanga ikishinda 3-1 dhidi
ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, siku ambayo alipasuka kwenye paji la
uso baada ya kugongana na Nahodha na kiungo wa wapinzani, Shaaban Nditi
mwishoni mwa mchezo.
Kutoka
hapo, Tambwe akakosa mechi mbili zilizofuata dhidi ya Azam FC Oktoba 16
timu hizo zikitoka sare ya 0-0 Uhuru na Oktoba 19 dhidi ya Toto
Africans Yanga ikishinda 2-0 Uwanja wa Kirumba, Mwanza kabla ya kutokea
benchi dakika za mwishoni kwenye mechi na Kagera Sugar Oktoba 22 Uwanja
wa Kaitaba, Bukoba timu yake ikishinda 6-2.
Na
baada ya Jumatano kutumia muda mfupi kufunga mabao mawili kwa jitihada
binafsi, Tambwe leo ameanzishwa pamoja na Mzambia Obrey Chirwa katika
safu ya ushambuliaji.
Kwa
ujumla kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Mbao FC ni; Deogratius Munishi
'Dida', Hassan Kessy, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent, Vincent
Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe, Obrey
Chirwa na Deus Kaseke.
Katike benchi wapo Benno Kakolanya, Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Donald Ngoma na Matheo Anthony.
Comments
Post a Comment