LIGI DARAJA LA KWANZA RATIBA YA LEO OCTOBAR 29


Image result for picha za DARAJA LA KWANZA
Mechi za Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2016/2017 zitaendelea tena leo Oktoba 29, 2016 kwa michezo minane ya makundi A, B na C.

Katika kundi A kutakuwa na michezo miwili ambako Polisi Dar itacheza na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam wakati Friends Rangers itasafieri hadi Tanga kupambana na African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Jumatatu Oktoba 31, mwaka huu kutakuwa pia na michezo miwili ya kundi hilo ambako Mshikamano na Ashanti zitachuana jijini Dar es Salaam kwenye kwenye Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini.

Kundi B kutakuwa na michezo mitatu kwa siku ya leo Oktoba 29, 2016 ambako Mlale itaikaribisha Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Kurugenzi ya Mafinga itakuwa mwenyeji wa Kemondo ya Morogoro kwenye Uwanja wa Uwambi huko Iringa ilhali Njombe Mji itacheza na Mbeya Warriors ya Mbeya huko Makambako.

Katika kundi hilo, KMC ya Dar es Salaam itacheza Jumatatu Oktoba 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.

Kadhalika Kundi C kutakuwa na mechi tatu. Mechi hizi ni kati ya Singida United itayocheza na Polisi Mara kwenye dimba la Namfua mjini humo wakati kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Polisi itakuwa mwenyeji wa Rhino ya Tabora ilhali Panone ya Kilimanjaro itacheza na Mgambo JKT ya Tanga kwenye Uwanja wa Ushisirika mjini Moshi.

Comments