MAMBO YA KUFANYA KAMA KUNA MWANAMKE ANACHELEWA KUJIBU TEXT ZAKO

Unafukuzia mwanamke mzuri mnaanza kuzungumza. Mnachukua muda wa dakika 20 hadi 30 kuongea na yeye mara ya kwanza. Anapendeza na kuvutia, na unaona kama ni mwanamke ambaye ni yule aliyekuwa ndotoni mwako maishani mwako. Mazungumzo yenu yanaenda vizuri mpaka ukwamwomba namba yake.

Baadaye unajaribu kumtumia text na hazijibu. Labda mnaeza kuchat kwa madakika halafu baada ya hapa anakataa kujibu texts zako. Unabaki ukijiuliza maswali ni kitu gani ambacho umefanya ambacho umekosea. Ok labda anaweza kuwa yupo buzy unampa muda kiasi ajibu text zako...unangojea masaa, siku, wiki mpaka inafikia wakati unagundua kuwa amekupuuza. Kwa nini hajajibu text zako?

So kwa nini hakujibu text zako?
Katika situation nyingi ni kuwa sababu kuu ambayo amekataa kujibu texts zako ni kuwa haukumpendeza mara ya kwanza ulipokutana naye. Ok labda sababu nyingine inaweza ni kuwa ameibiwa simu yake wakati alipokuwa akitext na wewe barabarani ama kitu kingine kama hicho, lakini hapa acha tumakinike na hatua ya kwanza uliokutana naye...yaani first impression ambayo unakudana na mwanamke yeyote.

1. Hakikisha unampendeza mara ya kwanza unapokutana naye
Anaweza kuwa hana muda mrefu wa kukaa na wewe ili akutambue zaidi so kile kitu ambacho unahitaji kufanya ni kuwa lazima uuonyeshe upendo wako kwa kuwa mpole, mkarimu na mtulivu.
2. Taja sababu zako za kuongea na yeye
Mfano: Nimefurahia sana kuongea na wewe. Kusema kweli nimependa maonezi yetu machache. Nataka kwenda lakini naonelea wikendi nitakutext tukutane ili tuongee tena.
3. Hakikisha kuwa unamtumia text wakati ufaao
Ukiomba namba ya simu kwa mwanamke inamaanisha kuwa wewe umeonyesha intrest kwake vilevile mwanamke akikupatia namba yake ya simu inamaanisha kuwa labda itakuwa amependezwa na wewe.
Wanawake wanapenda kuona wanababaikiwa na kufukuziwa.
ONYO: Hakikisha ya kwamba haupitishi zaidi ya siku tatu kwani anaweza kukusahau kwa haraka ama kuona unampotezea wakati wake.

4. Kitu cha kuandika kwa text yako ya kwanza
Messages za kwanza ambazo utazituma kwa mwanamke zitachangia pakubwa kuona kama wewe uko uko interesting ama unaboa. Unaweza kuuharibu mchezo mzima kama iwapo utaanza kumtext na mambo ambayo hayana manufaa kwake.

5. Jaribu kuhepa stori ambazo hazitafikia popote
Mara ya kwanza anaweza kukujibu lakini itafikia pahali atanyamaza. KUMBUKA: Siri kuu ya kumfanya mwanamke ajibu texts zako ni uwe makini kwake, yaani unamtext vtu ambavyo unajua yuko intrested navyo.

6. Weka wazi kuwa unataka mkutano
Acha stori za kumzungusha huku na huku kama wanaume wengine. Ukitaka akujibu text zako hakikisha ya kuwa unadhihirisha azma yako kwa kumwambia kuwa unataka kukutana naye.

7. Usikate tamaa
Kuna wanaume wengine kama wamekataliwa kujibiwa texts zao mara moja basi wanakasirika na wanaachana kabisa na kushungulika tena. Tatizo labda linaweza kuwa mwanamke anakupima akili aone bidii yako kwake.
KUMBUKA: Kuna sababu tofauti tofauti ambazo zinaweza kumfanya mwanamke kukataa kujibu texts zako. Labda umemtusi, hujampendeza, ni mwanamke mwenye haya nk. So hizi hatua zitategemea na vile imetokea katika situation yako.

Comments

Popular Posts