Mashabiki walio ng'oa viti uwanjani chelsea vs west ham mbaroni

 Saba mbaroni kwa kufanya ghasia na kung'oa viti uwanjani
Kumbe tabia ya mashabiki kuwa na ghadhabu na kung'oa viti siyo bongo tu, hata Ulaya wapo! Mashabiki waling'oa viti Chelsea ikinyukwa na West Ham

Saba wanashikiliwa na polisi baada ya ghasia zilizozuka baina ya mashabiki katika mechi ya Kombe la EFL kati ya West Ham United na Chelsea katika uwanja wa London Jumatano usiku.
Mashabiki wa mahasimu hao walipasuana katika mechi ambayo Wagonga nyundo walishinda 2-1 dhidi ya Chelsea, sarafu na viti vikirushwa uwanjani.
Shirikisho la soka la Ligi ya Uingereza kadhalika Shirikisho la Soka FA, yameanza kufanya uchunguzi kufuatia ghasia hizo.
Waraka uliosomeka: "EFL inalaani vikali tabia ya kundi dogo la mashabiki waliohusika na tukio hili baya ambalo hatuliungi mkono kabisa lililotokea jana usiku katika mechi baina ya Chelsea na West Ham United.
"Kwa sasa tunashughulika na klabu zote mbili, Shirikisho la Mpira wa miguu na polisi kubaini wale waliohusika kwenye tukio hilo na kuwachukulia hatua stahiki.

Comments