MCHINA APIGWA VIBAYA HADI KUZIMIA NA DULLA MBABE
Bondia chipukizi kutoka Tanzania Abdallah Pazi Dulla Mbabe alimrambisha sakafu mwenzake kutoka China Zheng Chengbo katika pigano kali lililofanyika usiku
wa Ijumaa katika ukumbi wa Diamond Jubilee mjini Dar es Salaam.
kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania ngumi nzito iliorushwa na Dulla ilimwangusha mpinzani wake na kumfanya kushindwa kuendelea na pigano hilo la uzani wa Light Heavy.
Pazi alianza pigano hilo kwa kasi na kufanikiwa kumwangusha bondia huyo wa China kwa sekunde kadhaa.
Hatahivyo Chengbo aliamka na kuendelea na pigano.
The Citizen linasema kuwa bondia huyo wa Tanzania alifanikiwa kumweka Chengbo katika kona na kumrushia makonde makali akimwacha akitokwa na damu chungu nzima katika pua.
Ni wakati huohuo ambapo bondia huyo alishindwa kunyanyuka kutoka sakafuni ndiposa refa akamaliza pigano hilo na kumpatia ushindi wa Knock-out Dulla.
Bondia huyo sasa ameshinda mapigano 14 ,13 yakiwa katika njia ya Knockout na kushindwa mara tatu
Comments
Post a Comment