MISS TANZANIA ATOA NENO BAADA YA KUCHAFULIWA MITANDAONI
Baada tu ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Miss Tanzania mwaka 2016, Mrembo Diana Lukumay
alianza kupokea msg za taarifa zilizosambazwa
mitandaoni kuonyesha
kwamba alifeli kidato cha nne lakini pia pamoja na hayo bado CV yake
ilionyesha anayo degree.
Diana ameamua kuweka kila kitu wazi kwa kusema ‘Jina
langu ni Diana Loi Lukumay, mmasai na umri wangu ni miaka 18,
nilizaliwa Arusha Mount Meru Hospital na ni mtoto wa tatu kwenye familia
ya watoto wanne’
‘Nilisoma
shule ya msingi ya serikali Levolosi 2005-2011, sekondari ya kutwa ya
serikali Arusha 2012 -2015, matokeo ya kidato cha nne nilipata darala
la pili… nilichaguliwa kujiunga na kidato cha tano mchepuo wa Sanaa
kwenda shule ya Wasichana Bwiru Mwanza‘
‘Kwakuwa nilikua tayari nipo
kwenye tasnia ya urembo niliamua kutojiunga na masomo hayo kwakuwa
yalishaingiliana na ratiba za mashindano haya katika ngazi ya kitongoji
ambapo nilijiunga na kambi ya Miss Ubungo 2016/2017)‘ – Diana
‘Baada ya
kuahirisha masomo ya kidato cha tano niliomba kujiunga na masomo ya
ngazi ya cheti kozi ya maswala ya kodi katika chuo cha usimamizi wa
fedha ambapo mpaka masomo yanaanza mwanzoni mwa October 2016 tayari
nilikua kwenye kambi ya Miss Tanzania, mafanikio ambayo niliyapata baada
ya kuibuka mshindi na kutangazwa kuwa lete Raha Miss Kinondoni
2016/2017′
‘Juhudi zangu hazikuishia hapo,
nilipotangazwa mshindi sikubweteka na taji hilo bali niliendelea na
kazi zangu za kijamii katika jamii yangu ya kimasai‘ – Diana
Comments
Post a Comment